Rukia hadi maudhui

Kwa biashara za Tanzania

Link moja. Bidhaa zako zote.

Acha kutuma picha zilezile kila siku. Weka bidhaa zako mahali pamoja, shiriki link moja, na mteja aagize moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Tengeneza link yangu

Bure kuanza. Hakuna kadi ya benki.

Link yako itakuwalinkiyangu.co.tz/duka-lako

“Una nini na bei gani?”

Swali lilelile kila siku. Picha zilezile zinatumwa upya, bei zilezile zinarudiwa — mazungumzo moja baada ya jingine. Bidhaa zako zipo, ila zimetawanyika kwenye post, story na albamu za picha.

Hatua tatu, si zaidi

  1. Jisajili

    Jina la biashara, namba ya simu, nenosiri. Unapata link yako ya kudumu papo hapo.

  2. Ongeza bidhaa

    Picha, jina, bei. Bidhaa moja inachukua chini ya sekunde 30 kwenye simu yako.

  3. Shiriki link

    Iweke kwenye bio ya Instagram, status ya WhatsApp au TikTok. Link haibadiliki kamwe.

Kila kitu duka la mtandaoni linahitaji

  • Oda zinaishia WhatsApp

    Mteja anabofya “Agiza” na WhatsApp inafunguka na ujumbe tayari umeandikwa: jina la bidhaa, bei na link yako.

  • Ukurasa ulioandaliwa tayari

    Kila katalogi hutumia muundo mmoja ulioundwa kwa simu na mtandao wa polepole. Weka nembo, jina na picha zako — mpangilio tumeuandaa.

  • Takwimu unazoweza kutumia

    Ona watu wangapi wamefungua ukurasa, bidhaa zipi zinabofywa zaidi, na oda ngapi zimeanzishwa.

  • Bei na stoku mkononi

    Badilisha bei au zima bidhaa iliyoisha popote ulipo. Mteja anaona mabadiliko mara moja.

  • Makundi ya bidhaa

    Panga bidhaa kwenye makundi ili mteja apate anachotafuta bila kupitia ukurasa mzima.

  • Nyepesi kwenye bando

    Ukurasa unafunguka chini ya sekunde tatu hata kwenye mtandao wa 3G, na picha zimepunguzwa ukubwa.

Panga kulingana na duka lako

  • Bure

    Hadi bidhaa 5

    Kwa anayeanza au mwenye bidhaa chache maalum.

  • Inapendekezwa

    Ya kawaida

    Hadi bidhaa 100

    Kwa duka linalouza kila siku na lina orodha inayokua.

  • Premium

    Bidhaa bila kikomo

    Kwa duka kubwa lenye orodha ndefu na makundi mengi.

Bei za mipango ya malipo zitatangazwa kabla ya uzinduzi.

Duka lako lina link yake tayari.

Jisajili bure, ongeza bidhaa tano, na uone inavyofanya kazi.